Kikosi cha Simba SC kimrejea jijini Dar es salaam kikitokea Dodoma kilipokuwa kinakabiliwa na mchezo wa Mzunguuko wa 21 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Mchezo huo uliopigwa jana Jumapili (Januari 22) ulishuhudia Simba SC ikiibuka na ushindi wa 1-0, bao likifungwa na Mshambuliaji kutoka DR Congo Jean Baleke dakika ya 45+1.

Meneja wa Habari na Mawasilino Ahmed Ally amesema baada ya kikosi chao kuwasili, wachezaji watakua na mapumziko kwa siku ya leo, na kesho Jumanne (Januari 24), watarejea kambini kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Jumamosi (Januari 28), Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ahmed amesema wanaupa umuhimu mkubwa mchezo huo, kutokana na malengo waliojiwekea msimu huu, ili kuhakikisha wanarejesha heshima ya mataji iliyowaponyoka msimu uliopita.

“Hatujawahi kutokuwa na malengo katika Mashindano yote tunayoshiriki, ndio maana tumeamua kesho wachezaji wote warejee kambini ili kuanza maandalizi ya kuivaa Coastal Union JAnuari 28,”

“Maandalizi yetu yataanza katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena pale Bunju.” amesema Ahmed Ally
Ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC, unaiwezesha Simba SC kufikisha alama 50 zinazoendelea kuiweka kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikitanguliwa na Young Africans iliyo kileleni kwa kumiliki alama 53.

Simba SC imeshacheza michezo 21 ya Ligi Kuu hadi sasa, huku Young Africans ikicheza michezo 20.

Abdallah Bares anukia Tanzania Prisons
Watanzania hunywa Chai daraja la tano