Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wameshindwa kufurukuta mbele ya Mlandege FC katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliocheza leo Ijumaa (Januari 07).

Mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Aman Kisiwani Unguja-Zanzibar umeshuhudia timu hizo zikimaliza dakika 90 kwa sare ya 0-0.

Sare hiyo imeivusha Simba SC hadi katika Nusu Fainali ya Michuano hiyo, baada ya kufikisha alama 4 na mabao mawili ya kufunga.

Mlandege FC nao wamemaliza na alama 4 lakini wana bao moja la kufunga, hivyo wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi B.

Timu zilizotinga nusu fainali ni Azam FC, Namungo FC, Young Africans na Simba SC zote kutoka Tanzania Bara.

Hatua ya makundi itakamilishwa kesho kwa mchezo wa Kundi A ambapo Azam FC itacheza dhidi ya Yosso Boys.

Mwigizaji maarufu wa Holywood Sidney Poitier afariki dunia
Ufunguo wa Gereza la Mandela, Tunu Afrika Kusini