Vita ya kuwania Taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, imeendelea kupamba moto kati ya Simba SC na Young Africans huku alama 08 zikizitofautisha klabu hizo katika msimamo.

Simba SC inayotetea Taji hilo kwa mara ya tano ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 49, huku Young Africans inayolisaka Taji la Ligi Kuu kwa msimu wa tano mfululizo ikiwa kileleni kwa kufikisha alama 57.

Simba SC wanaamini tetesi za usajili wa Bernard Morrison kwenda Young Africans zinazoendelea katika mitandao ya kijamii ni sehemu ya Propaganda za vita ya kuwania Ubingwa msimu huu.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amethibitisha kushtukiwa kwa Propaganda hizo zinazotumiwa na Upande wa pili, huku akisistiza kuwa klabu yao haitoyumbishwa na Popaganda hizo.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutoa ufafanuzi wa Proganda hizo kwa kuandika: Mmeanza cheap propaganda kuhusu wachezaji wetu ?

Sisi tunafurahi kuona mnawawaza wachezaji wetu hii inamaana kuwa mnakubali kuwa tunawachezaji ambao wanaweza kuwasaidia

Sisi tunawaza kusajili wachezaji kutoka Raja Casablanca nyie mnawaza kusajili mchezaji kutoka Simba kila mtu anamuwaza mkubwa wake

Lakini tuwaambie tuu hatubabaishwi na propaganda rahisi kama hizo, focus yetu ni kwashusha hapo kileleni

Na kama haitoshi uyo mchezaji mnaemzungumzia tunaweza kumsajili halafu tukawapa kwa mkopo

Hamtutoi relini kwa propaganda za nursery school

Ushindi dhidi ya Mtibwa, Kocha KMC FC aitaja Real Madrid
Bernard Morrison bado anaitaka Simba SC