Mabingwa Tanzania Bara na Wawakilishi katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Simba SC, wameanza vizuri michuano hiyo kwa kushinda ugenini mabao 2-0.

Simba SC imecheza dhidi ya Jwaneng Galaxy mjini Gaborone, Botswana leo Jumapili (Oktoba 17).

Mabao ya ushindi ya Wekundu hao wa Msimbazi yamefungwa na Nahodha na Mshambuliaji John Raphael Bocco dakika ya 02 na ya 05.

Ushindi huo wa ugenini ni mwanzo mzuri kwa Simba SC ambayo itakuwa mwenyeji wa mchezo wa mkondo wa pili utakaounguruma siku ya Ijumaa (Oktoba 22) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba SC inatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam wakati wowote kuanzia kesho, kwa usafiri maalum wa ndege ya kukodi.

Morena: Simba ni dhaifu, tutaifunga kwao
Wanufaika wa HESLB waula