Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC kupitia ukurasa wao wa Instagram, wamethibitisha kuwa kikosi cha klabu hiyo kitaondoka jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya 2021/22.

Simba SC wametoa taarifa hiyo, wakitanguliwa na watani zao wa jadi Young Africans, ambao mapema leo asubuhi walithibitisha taarifa za safari ya kikosi chao kuelekea Morocco.

Simba SC itaweka Kambi nchini humo, kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ‘CAF’.

Simba SC itakuwa nchini Morocco hadi mwishoni mwa mwezi huu, kisha itarejea nchini kwa ajili ya Simba Day (Agosti 28).

PICHA: Simba SC yaanza safari ya Morocco
Taliban yabeba jiji la sita Afghanistan, ‘Marekani kimya’