Baada ya kiosi cha wekundu wa Msimbazi Simba kupoteza mchezo wao dhidi ya Azam FC kwa goli 1-0 juzi, leo Jumatatu ya January 8 2018 walikuwa wanatupa karata yao ya mwisho dhidi ya URA ya Uganda.

Simba walikuwa nafasi ya tatu wakiwa na point nne, Azam FC wakiongoza Kundi kwa kuwa na point 9 wakifuatiwa na URA waliokuwa na point saba, hivyo ni wazi mchezo wa leo wa URA dhidi ya Simba SC ulikuwa kama ni fainali kwa timu hizo kwani Simba alihitaji ushindi ili afuzu kucheza nusu fainali huku URA akihitaji sare.

Bahati haikuwa kwa Simba na dakika ya 48 Kalama Deboss akapachika goli la ushindi kwa URA lililodumu kwa dakika zote 90 na kufanya ubao wa matokeo usomeke 1-0.

Hata hivyo nyota wa Simba Shiza Kichuya aligoma kukaa kwenya benchi la timu yao baada ya kocha kumtoa dakika ya 53 na kuingia MO Ibrahim.

Kwa mantiki hiyo Simba imeondoshwa kwenye michuano hiyo na imeendelea kusalia katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi A.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 9, 2018
Mbowe, Lowassa wamtembelea Kingunge Muhimbili