Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imefanya mabadiliko ya tarehe ya mchezo wa watani wa jadi katika soka la bongo Simba na Young Africans ambao kwa ratiba ya awali ulipangwa kuchezwa April 07.

Afisa mtendaji mkuu wa bodi hiyo Boniface Wambura leo ametangaza mabadiliko hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya shirikisho la soka nchini TFF.

Wababe hao katika soka la bongo wamepangiwa kukutana April 29 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo ambao Simba watakuwa mwenyeji.

Mchezo wa mkondo wa kwanza kwa wawili hao ulichezwa Oktoba 28 2017 kwenye uwanja wa Uhuru na kumalizika kwa sare ya bao moja kwa moja, huku wafungaji wa mabao hayo wakiwa ni Shiza Kichuya upande wa Simba na Obrey Chirwa kwa Young Africans.

Mabadiliko ya ratiba kwa michezo mingine kiporo cha mchezo wa Njombe Mji FC dhidi ya Simba kitachezwa Aprili 3 2018 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Mchezo huo ulioahirishwa ili kuipa nafasi Simba ya kujiandaa na mechi dhidi ya Al Masry katika Kombe la Shirikisho, sasa umepangwa tarehe tajwa hapo juu.

Tarehe zilizopangwa upya kwa michezo mingineya Simba

Aprili 9: Mtibwa vs Simba

Aprili 20: Lipuli FC vs Simba

Aprili 29: Simba vs Yanga

Nao mchezo wa Mtibwa Sugar dhidi ya Young Africans umepangwa kufanyika Mei 09 katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro.

Mchezo huo uliahirishwa ili kuipa nafasi Young Africans kufanya maandalizi ya kucheza na Township Rollers FC kwenye mshike mshike wa ligi ya mabingwa barani Afrika.

Lionel Messi ampeleka Neymar Manchester City
Telstar 18 wamchukiza David de Gea