Klabu ya Simba imeamua kuongeza kasi zaidi katika suala la kupata kocha mpya.

Simba imeamua kufanya hivyo baada ya juhudi zake za kumnasa Kalisto Pasuwa wa Zimbabwe, kugonga mwamba maana amekubali kubaki na timu yake ya taifa ya nchi hiyo ambayo ameiwezesha kufuzu fainali za mataifanya Afrika za mwaka 2017.

“Tunaona suala la kocha liwe namba moja. Wachezaji tayari tumeanza kusajili vizuri tu,” kilisema chanzo cha uhakika.

“Lakini ni vizuri kuangalia kuhusiana na kocha maana yeye anatakiwa kuja mapema na kuanza na kikosi.

“Kweli juhudi zinaendelea kwa nguvu kabisa. Lakini ni suala la kusubiri uhakika pia makubaliano,” kiliongeza chanzo.

Taarifa nyingine zimesema, kama watachelewa kupata kocha, bado Kocha Msaidizi na kaimu kocha mkuu, Jackson Mayanja ataianza kazi hiyo ya maandalizi wa mwanzo wa msimu.

Ronaldo Aonyesha Dharau Dhidi Ya Iceland, Mashabiki Wamshambulia
Ratiba Ya Ligi Ya England Msimu Wa 2016-17 Yaanikwa Hadharani