Beki wa pembeni kutoka nchini Burundi  Emiry Nimubona ameondoka Dar es salaam na kurejea mjini Bujumbura huku akiaga rasmi kwamba hatarudi kuichezea tena timu hiyo kwani wamemamlizana kila kitu.

Nimubona ndiye mchezaji pekee wa kigeni wa Simba ambaye alibaki Dar es Salaam akisubiri haki zake pamoja na barua ya kuachwa huru huku wenzake wakiwa wameondoka kwa gharama zao.

Tayari Simba haitakuwa na mchezaji huyo msimu ujao wa Ligi Kuu Bara pamoja na Raphael Kiongera, Brian Majwega na Justice Majabvi wakati Juuko Murshid na Hamis Kiiza uamuzi bado haujatolewa rasmi ingawa nao wanatajwa kuachwa.

Nimubona amesema kuwa amekutana na changamoto nyingi za kisoka hasa tangu timu hiyo ipoteze mechi ya Kombe la FA ambapo walianza kutuhumiwa kwa kucheza chini ya kiwango.

“Katika soka kuna changamoto nyingi lakini hii ya sasa ilizidi, nimegundua kwamba Simba wakikuchoka wanaanza kukutafutia sababu, siku za hivi karibuni nimekuwa nikijibiwa vibaya na baadhi ya viongozi ila nilivumilia kwani najua maisha yangu yakoje katika soka.

“Sikutaka kuondoka bila kujua hatima yangu, nilikutana nao tukajadili ingawa mazungumzo yao niligundua tu kuwa hawanitaki, ndipo niliomba barua ya kuachwa huru na wamenipa. Hivyo naondoka Simba nikiwa siwadai kwani wamenipa haki zangu na wao hawanidai naenda kutafuta maisha sehemu nyingine,” alisema Nimubona.

Awali Nimubona alikutana na changamoto ya namba kutoka kwa Hassan Kessy ambaye pia ameondoka na kusaini Yanga lakini baadaye alikumbana pia na changamoto ya kuondolewa kikosini walipogoma kwenda Songea kucheza mechi yao na Majimaji kwa madai ya kutaka walipwe mshahara wao.

Simba ipo kwenye mchakato wa kutafuta beki wa kulia ambaye ataziba vilivyo pengo lililoachwa na Kessy pamoja na Nimubona

Zlatan Ibrahimovic Kusajiliwa Kabla Ya Euro 2016
Hatari: Mrembo anyonyoka nywele kwa Kusuka ‘Weave kichwani’