Wakati Yanga ikiwa kwenye hekaheka za usajili imeripotiwa kuwa uongozi wa Simba wameanza kufanya mawasiliano na winga wa kimataifa wa Msumbiji na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Luis José Miquissone.
Taarifa zinasema Simba imeanza mazungumzo na winga huyo anayecheza kwa mkopo UD Songo ya Msumbiji ili kumsajili katika dirisha dogo la usajili ambalo tayari limeshafunguliwa Jumatatu ya wiki hii.
Awali Muquussone alikuwa akihusishwa kusajiliwa na Yanga ambao usajili wao umeanza kwa kasi dirisha hili.
Haijaeleweka mpaka sasa watani wao wa jadi Yanga wamefikia naye hatua ipi ya mzungumzo lakini taarifa za ndani zinasema bado wanaendelea kufuatilia saini yake.

Video: Katibu mkuu Chadema aacha utata, Magufuli azidi kufanya maajabu
FIFA yashusha neema Tanzania