SIMBA inakabiliwa na mambo mawili muhimu, mechi na Al Masry ya Misri kwenye Kombe la Shirikisho pamoja na ligi kuu, sasa kocha mkuu wa kikosi hicho Pierre Lechantre, ameandaa mikakati mizito kuhakikisha jiwe moja linaua ndege wawili huku akitoa angalizo kuwa kuwakabiri Waarabu inahitaji akili nyingi si kama Gendarmarie.
Asilimia 90 iko wazi Simba itacheza na Al Masri Kombe la Shirikisho baada ya kuwafunga Green Buffalo ya Zambia mabao 4-0 mechi ya kwanza, lakini pia wikiendi hii watacheza mechi ya ligi na Mbao FC.
Kutokana na hilo, Lechantre amesema, mambo hayo mawili yote ni muhimu na yote lazima afanikiwe ili kukamilisha malengo yake.
“Al Masry ni timu bora Misri wanacheza kwa mipango na kwa nafasi, nafikiri mechi tuliyocheza na Gendarmarie si ya kufananisha na Al Masri kwa sababu uwezo wao ni tofauti,” alisema Lechantre.
ASFC kuendelea kesho
Video: JPM, Kenyatta wasema wapo sawa, wawaagiza mawaziri kutatua tofauti ndogondogo zilizopo

Comments

comments