Klabu bingwa ya Ligi kuu ya soka nchini Tanzania, Simba imeendelea kufanya usajili kwa wachezaji ambao walikua wakiwahitaji  kwaajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hiko.

Simba imemsajili mlinzi wa kati Kennedy Wilson Juma akitokea katika kikosi cha walima Alizeti cha Singida United Fc ambaye alionesha kiwango kikubwa msimu uliopita na kuisadia timu yake kusalia kwenye Ligi kuu ya soka ya Tanzania bara.

Kennedy amesaini mkataba wa miaka miwili ili kuweza kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao na unaofuata ambapo anatarajiwa kwenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi ambapo atashirikiana na Erasto Nyoni na Sergie Pascal Wawa ambaye inasemekana yupo mbioni kutimka kwenye kikosi hiko chenye maskani yake iliyopo Kariakoo mtaa wa Msimbazi jijini Dar Es Salaam.

Ikumbukwe msimu uliopita Simba ulikuwa wa mafanikio kwa upande wao ambapo walifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mara ya pili mfululizo pamoja na kufika hatua ya robo fainali katika ligi ya mabingwa barani Afrika pasi na kutopoteza mchezo wowote katika uwanja wake wa nyumbani nchini Tanzania.

 

Serikali yaokoa mabilioni uendeshaji mashauri ya madai
Nape ashauri kuwepo ubunifu katika ulipaji kodi