Klabu ya Simba imefanikiwa kumsajili kiungo wa Mtibwa Sugar, Muzamil Yassin kwa Mkataba wa miaka miwili na sasa inahaha kukamilisha usajili wa kiungo mwingine wa timu hiyo ya Morogoro, Shizza Kichuya.

Muzamil anakuwa mchezaji wa tatu kusaini Simba, baada ya beki Emmanuel Semwanza na kiungo Jamal Mnyate wote kutoka Mwadui ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amekataa kutaja wachezaji waliosajiliwa hadi sasa, kwa madai kuwa watatangaza rasmi kesho (Leo), lakini tayari imeshafahamika Semwanza, Mnyate na Muzamil ndiyo wamesaini kati ya sita wanaowataka.

Wengine ambao Simba ilikuwa inahaha kukamilisha usajili wao ni winga machachari wa Mtibwa Sugar, Shizza Ramadhani Kichuya, Salim Kimenya na Jeremiah Juma wa Prisons.

“Siwezi kukuambia tumemsajili nani na nani, ila nataka nikuhakikishie tumekwishapata saini sita za askari shupavu, weledi na waaminifu, watakaorejesha heshima ya Mnyama msimu ujao,”alisema Hanspoppe.

Alipoulizwa kama saini hizo ni za wachezaji wa nyumbani tu au na wa kigeni pia, Hans Poppe alisema; “Mtajulishwa kesho (Leo).

Hazard: Sikua Miongoni Mwa Wasaliti Wa Jose Mourinho
Model wa video ya Nuh Mziwanda amvimbia Shilole