Klabu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Magoli ya Simba yalifungwa na Paul Bukaba dakika ya 52 pamoja na Meddie Kagere dakika ya 56 kwa mkwaju wa penati.

Ushindi huo umeifanya Simba SC kufikisha alama 54 nafasi ya tatu katika michezo 21 ya Ligi Kuu ikishinda michezo 17, sare michezo 3 na kupoteza mchezo 1, Azam FC ikiwa nafasi ya pili kwa alama 59 katika michezo 28, ikishinda michezo 17, sare michezo 8 na kupoteza michezo 3, huku Yanga SC ikiendelea kusalia kileleni kwa alama 67 katika michezo 28 ikishinda michezo 21, sare michezo 4 na kupoteza michezo 3.

Simba waliingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu za kutoka kufuzu kucheza robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya AS Vita.

Huwenda wangeweza kupoteza mchezo huo dhidi ya Ruvu Shooting au kutoka sare kutokana na uchovu dhidi ya game yao ya mwisho ya makundi ya CAF Champions League, lakini Simba SC wameendeleza vichapo kwa kuifunga Ruvu Shooting magoli 2-0.

Wakati Simba SC wanaendelea kuwa nafasi ya 3 wakiwa na point 54, bado wana viporo 7 vya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL).

Video: HII HAIJAWAHI KUTOKEA: Simba yaweka Rekodi | Maelfu Uwanjani | Yawaweka Vifua mbele Mashabiki wake

Maono ya mchungaji kifo cha Kibonde yamtia mikononi mwa polisi Oysterbay
Video: Maalim Seif 'apindua meza' ACT - Wazalendo, Tanzania yasaidia nchi 3