Mshambuliaji  machachari wa Mwadui Jamal Simba Mnyate amemwaga wino kuwatumikia Wekundu Wa Msimbazi Simba.

Inaelezwa kwamba Mnyate amesaini mkataba wa miaka miwili na amesajiliwa kwa kitita cha shilingi milioni 15.

Ikumbukwe kwamba, Manyate ndiye aliwaua Simba kwa kuifungia timu yake ya Mwadui goli la pekee lililoipa ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara raundi ya pili uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

JAMAL MNYATEJamal Simba Mnyate akimiliki Mpira mbele ya beki wa pembeni wa timu ya Simba Mohamed Hussein wakati wa mchezo wa ligi kuu ambao ulishuhudia Mnyama akifungwa bao moja kwa sifuri, lililofungwa na mshambuliaji huyo alipokua Mwadui FC.

Video: Serikali imepata gawio la bilioni 23 la ubia kutoka Puma, NMB na Tiper
AC Milan Wamvuta Manuel Pellegrini Kimya Kimya