Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wameibomoa Young Africans kwa kumchukua mchua misuli anayefahamika kwa jina la Farid raia wa afrika Kusini.

Farid alionekana katika tamasha la Simba Day jana Jumapili (Septamba 19) wakati wa kutambulishwa kwa viongozi wa Benchi la Ufundi na wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya msimu wa 2021/22.

Rasmi Farid alionekana hadharani jana Jumapili, alipoongozana na benchi la ufundi na kwenda kukaa nao pamoja kwenye sehemu yao maalum.

Farid amedumu na Young Africans kwa takribani misimu miwili akitoa huduma ya kuchua misuli wachezaji wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.

kabla ya kuajiriwa kwa Farid klabuni hapo, Simba SC haikuwa na mchua misuli bali walikuwa na Adel Zrane ambaye yeye ni mtaalamu wa viungo.
Ikumbukwe kuwa Farid alipokuwa Young Africans alikuwa na kitanda maalum ambacho alikuwa anatumia kuchua misuli wachezaji.

Pele: Ninaendelea vizuri
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 20, 2021