Ligi Kuu soka Tanzania Bara imeendelea hii leo kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali huko Kaitaba Mkoani Kagera, Klabu ya Simba imechomoza na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Kagera Sugar,

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa mechi hiyo imemalizika kwa matokeo hayo ambayo yanaifanya timu ya Simba kukwea kileleni kwa jumla ya pointi 32.

Aidha, mabao ya Simba yamefungwa wachezaji Said Ndemla aliyefunga goli la kwanza huku John Bocco akipigilia msumari wa pili.

Katika mchezo mwingine uliopigwa hii leo ni kati ya timu ya Majimaji FC dhidi ya Singida United, ambapo timu hizo zimetoka suluhu kwa kufungana goli 1- 1.

 

Mbowe ainyooshea kidole NEC
Wananchi kushuhudia chimbuko la binadamu