Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Klabu ya Soka ya Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa watani wa jadi uliopigwa kwenye dimba la taifa jijini Dar es salaam.

Simba imebeba pointi zote tatu kupitia bao la Meddie Kagere ambaye alifunga dakika ya 72 akipokea pasi safi kutoka kwa nahodha wa timu hiyo, John Bocco na kumalizia kwa kichwa.

Baada ya ushindi huo wa Simba, klabu ya Yanga imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 58 wakati Simba wanajivuta kutoka nafasi ya 5 hadi ya 3 wakiwa na pointi 39.

Aidha, tayari Yanga imeshacheza mechi 24 huku Simba wakicheza mchezo wao wa 16 msimu huu katika ligi ambayo ipo kwenye mzunguko wa 27 kwaa baadhi ya timu.

Kwa upande mwingine klabu ya Yanga ambayo imetoka kuadhibiwa na TFF kwa kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, itakuwa inasubiri adhabu hiyo tena baada ya leo kuingia tena uwanja wa taifa kwa kutumia mlango usio rasmi.

 

Hapo kale: Mambo sita ya Malkia Elizabeth II usiyoyajua
Hatufundishi askari wetu kuua watu- Kangi Lugola