Mabingwa wa Soka Nchini Klabu ya Simba kupitia kwa kocha wake msaidizi, Denis Kitambi amesema kuwa aina wa uchezaji utabadilika kidogo kutoka wanavyocheza kwenye ligi kuu ili kuendana na matakwa ya Ligi ya mabingwa.

“Lazima tuhakikishe tunapata matokeo mazuri ugenini na nyumbani lakini katika mchezo huu ni lazima tubadilike kidogo kutokana na utofauti wa mchezo huu ukilinganisha na michezo ya ligi kuu maana JS Sauora tuliwafunga nyumbani nao watataka kutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani,”amesema Kitambi.

Aidha, Simba inacheza na JS Saoura leo Jumamosi saa 4:00 usiku wakiwa katika nafasi ya pili na pointi 6 na endapo watashinda watafikisha pointi 9 huku wakisubiri matokeo ya AS Vita dhidi ya Al Ahly na kama mchezo huo utaisha kwa sare watakuwa wamefuzu robo fainali.

Hata hivyo, Simba wameondoka kwenye mji wa Algiers kwenda Béchar ambako ndipo utachezwa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni mechi ya tano kundi D.

Video: Sasa ni Lowassa vs Chadema, Kibonde kuzikwa alipolala mkewe
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 9, 2019