Mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Simba Sc imemleta kocha mpya raia wa Ubelgiji, Patrick Aussems ambaye amekuja kuchukua nafasi ya Pirre-Lechantre aliyeachana na klabu hiyo hivi karibuni.

Patrick Aussems, 53 aliwasiri nchini jumapili iliyopita na kufanikiwa kushuhudia mchezo wa pili wa Simba kwenye kombe la Kagame dhidi ya Rayon Sports  ambapo Simba ilishinda 2-1, Pia hapo jana kocha huyo alikuwepo uwanjani kushuhudia  Simba ikitoka sare na Singida United.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa kocha huyo yupo katika mazungumzo ya mwisho na uongozi wa klabu ya Simba kabla ya kuingia makubaliano ya kuifundisha timu hiyo ambayo inatarajiwa kuwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao.

Aidha, Kocha huyo anatajwa kuwahi kuzifundisha klabu tofauti zikiwemo ES Troyes AC na Stade De Reims za Ufaransa ,mabingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2012, AC Leopards ya DR Congo pamoja na timu ya taifa ya Nepal.

Patrick Winand Aussems , alikuwa mchezaji kabla ya kuwa kocha akicheza nafasi ya ulinzi na kufanikiwa kuchezea vilabu vikubwa barani ulaya zikiwemo Standard Liege, KRC Gent na RFC Seraing za Ubelgiji, pamoja ES Troyes AC ya Ufaransa.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 6, 2018
Biashara united yatambulisha kocha mpya