Mkuu wa Habari klabu ya Simba, Haji Manara ametangaza rasmi ujio wa kocha mkuu mpya kutoka Ufaransa Pierre Lechantre ambaye ataanza kazi yake mara moja akisaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo

Kocha Lichantre ameshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani ikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroon kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.

Kocha huyo pia amewahi kupata tuzo ya kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi, Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.

.

Azam FC Yavutwa jezi Songea
Mambosasa akanusha agizo la vimini na viduku