Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wamewasili jijini Dar es salaam wakitokea Jijini Mbeya walipokua na shughuli ya kupambania alama tatu dhidi ya Mbeya City Jana Jumatatu (Januari 17).

Simba SC ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine huku bao la Ushindi wa Mbeya city likipachikwa wavuni na Mshambuliaji Paul Nonga dakika ya 20.

Baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Ahmed Ally amesema maandalizi ya kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar yanaanza mara moja, na wanatarajia kupata ushindi kwenye mchezo huo.

Ahmed amesema wanatambua Mtibwa Sugar watakuwa wamejawa na Morari baada ya kuona Simba SC imepoteza ugenini dhidi ya Mbeya City, lakini amewataka wajipange kwa sababu hasira za jijini Mbeya zitawashukia.

Kuhusu uhakika wa wapi mchezo utakapochezwa dhidi ya Mtibwa Sugar, Ahmed amesema hadi sasa hawana uhakika ni wapi watacheza mchezo huo, licha ya taarifa kuelekeza huenda wakakipiga na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Manungu Complex.

May be an image of 1 person, playing a sport and text that says "INBC PREMIER LEAGUE MTIBWA SUGAR SIMBA SC SIMBA PORTSCLU resa JUMAMOSI 22.1.2022 SAA 10:00 JIONI MANUNGU STADIUM TURIANI, MOROGORO ಕ LX3N H E"

Hata hivyo tayari Simba SC imeshathibitisha mchezo huo utachezwa Uwanja wa Manungu Complex, Mkoani Morogoro baada ya kuweka taarifa ya mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Waziri Ummy aja na kasi mpya
Tanzania kusikika tena Kimataifa