Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya mchezaji wake wa zamani Abel Dhaira ambae amepata ugonjwa wa kansa ya tumbo.

Dhaira ambae ni golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda na anayechezea klabu ya IBV Vestmannaeyiar ya Iceland alipata kuichezea klabu yetu ya Simba kwa mafanikio makubwa miaka michache iliopita.

Klabu imepokea taarifa za ugonjwa huo kwa taharuki kubwa na inaungana na Dhaira na familia yake kwenye kipindi hiki kigumu cha maradhi hayo makubwa

Tunaamini licha ya matibabu atakayoyapata kipa huyo pia nguvu ya Mwenyezi Mungu inahitajika katika kumponyesha nyota wetu mahiri Abel Dhaira.

Imetolewa na Haji Manara
Mkuu wa habari
Klabu ya Simba

Simba Nguvu Moja

Video Mpya: Unconditionally Bae - Saut Sol Feat. Ali Kiba
Magufuli awaruhusu mawaziri hawa wawili kufanya ziara nje ya nchi