Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amezitaka ofisi za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ziendelee kutoa elimu kwa Wananchi kuepuka uchafuzi wa vyanzo vya Maji na kula vyakula vilivyopoa au visivyoandaliwa katika Sehemu salama.

Simbachawene ameyasema hayo hii leo Machi 22, 2023 katika hafla ya uzinduzi wa Mpango Shirikishi wa Taifa, wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu (2023-2027), uliofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma na kuongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu itashirikiana na Wadau walioonesha nia ya kuungana na Serikali, ili kuhakikisha wakabiliana na ugonjwa huo.

Amesema, “tuwahakikishie Wadau wetu wa maendeleo World Health Organization – WHO, UNICEF, Save The Chidren na taasisi zote ambazo zimeonyesha nia ya kushirikiana na Setikali yetu kupambana na Ugonjwa huu wa kipindupindu,  tutakuwa bega kwa bega na ninyi ili kuzuia na kudhibiti ugonjwa huu.”

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene.

Hata hivyo, amesema Ugonjwa wa kipindupindu  unasambaa kwa kasi na wakati mwingine kuvuka hata mipaka ya nchi na kudai kuwa, “taarifa kutoka shirika la Afya Dunia inaeleza kuwa na mlipuko mkubwa wa Kipindupindu nchini Malawi ambapo hadi kufikia tarehe 15 Machi 2023 kulikuwa na jumla ya wagonjwa 53,925 na vifo 1,658 vilivyolewa taarifa.”

“Taarifa hii inatupa tahadhari ya mlipuko huo pia kuvuka mipaka na kuingia nchini kwetu hususani pale tusipo imarisha afua mbalimbali za kujikinga na kipindupindu kwa jamii zetu hususani kwa Mikoa inayopakana na nchi hiyo. Tetesi za kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu pia zipo kwa nchi nyingine tulizopakana nazo kama Msumbiji, DRC Congo, Zambia na Kenya,” amesema Simbachawene.

Aidha, ameongeza kuwa, “ni mategemeo yangu kuwa nchi imejiandaa kuhakikisha kuwa ugonjwa huu pale utakapokuwa umevuka mipaka na kuingia kwetu, nihimize pia Wizara ya afya kuongeza nguvu ya ufuatilaji, ili kuhakikisha wagonjwa na tetesi zote zinatolewa taarifa na kutibiwa mapema kwenye vituo vya kutolewa huduma kabla ugonjwa haujasambaa,” amesema Simbachawene

Simbachawene amebainuisha kuwa, mwaka 2015 hadi mwaka 2018 Mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu ulitoa uzoefu wa kukabiliana nao ingawa milipuko ya ugonjwa huu imepungua katika sehemu kubwa ya nchi na kwamba mlipoko wa sasa kuanzia Februari 19, 2023 – Machi 15, 2023 kuna taarifa za wagonjwa 60 (Ruvuma 1, Kigoma 7, Katavi 34 na Rukwa18).

Wananchi Bukoba waanza mapambano dhidi ya Marburg
Dkt. Mpango: Barabara Kabingo - Manyovu kuifungua Kigoma