Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, amemwambia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA, Dkt Anorld Kihaule, kama kazi imemshinda atoe taarifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznania Samia Suluhu Hassan ili nafasi hiyo ichukuliwe na mwingine.

Kauli hiyo ameitoa akiwa mkoani Iringa, na kumtaka Mkurugenzi huyo ajitathimini kuhusu suala la vitambulisho na kwamba kama anaona hawezi basi amwambie Rais Samia.

“Kwahiyo tangu nimeingia kwenye uwaziri kelele zote nilizopiga kwenye vitambulisho zimezalisha vitambulisho milioni 2 tu, na mimi siwezi kukubali ninachomwambia huyo Mkurugenzi Mkuu kama hii kazi imemshinda apewe kazi nyingine na hii aachie watu wengine, sawa ni mteule wa Rais, kama imemshinda amwambie,” Amesema Waziri Simbachawene.

Aidha Waziri Simbachawene amesema kuwa tangu ameanza kupiga kelele kuhusu vitambulisho vya NIDA hadi sasa vilivyozalishwa ni milioni 2 tu na kusema hali hiyo hawezi kuivumilia tena.

Halmashauri zatakiwa kutoa hati 100 kila mwezi
Ajira kwa wanawake zimepungua %4.2 duniani