Mashabiki wa timu ya Simba wamezua vuguru kubwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam punde baada ya Hamisi Tambwe kuipachikia timu ya Yanga goli moja (la kwanza).

Mashabiki hao wa Simba wamezua vurugu kupinga goli  hilo lililofungwa na Tambwe dakika ya 26, wengi wakiamini kuwa aliunawa mpira alipokuwa akiwaponyoka walinzi wa timu hiyo kabla hajafumania nyavu.

Polisi walilazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya baadhi ya mashabiki wa Simba waliokuwa waking’oa viti, hali iliyozua tafrani ya muda. Baadhi ya mashibiki walionekana kuzira na kuondoka uwanjani hapo.

Vurugu hizo zilizodumu kwa dakika tisa pia zilihusisha wachezaji ndani ya uwanja, hali iliyomlazimu muamuzi kumtoa nje Jonas Mkude kwa kadi nyekundu.

Mtanange huo wa watani wa jadi katika Ligi Kuu ya inayodhaminiwa na Vodacom unaendelea huku Yanga wakiongoza kwa goli moja hadi mapumziko huku Simba ikiwa na upungufu wa mchezaji mmoja.

Yanga wameongoza kwa kumiliki mpira (ball possession) kwa asilimia 55 dhidi ya asilimia 45 za Simba.

 

Video: Wanasheria Ukawa kupambana na Prof. Lipumba
Video: Ukawa wasema hawamtambui Prof. Lipumba, hawamtaki kwenye Umoja wao