Mwanariadha, Alfonce Felix Simbu amezidi kuing’arisha Tanzania kimataifa mara baada ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya IAAF2017 ChampionShip Marathon yanayofanyika jijini London nchini Uingereza.

Simbu ameshika nafasi ya tatu ambapo ametumia muda wa masaa 2:09:51 akiwa nyuma ya wafukuza upepo kutoka Kenya na Ethiopia ambapo,  Geofrey Kiriu kutoka Kenya ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa Tamirat Tola wa Ethiopia aliyeshika nafasi ya pili.

Aidha, mwanariadha huyo mwaka jana alishika nafasi ya tano katika mashindano hayo lakini maandalizi mazuri aliyoyafanya kwa mwaka huu yameweza kuzaa matunda ya kuongeza nafasi nyingine.

Hata hivyo, katika ushindi wa nafasi ya tatu, Simbu amejinyakulia medali ya shaba ,huku akiwa ni Mtanzania wa pili kushinda medali katika mashindano hayo ya Dunia baada ya Christopher Isegwe mwaka 2005 kutunukiwa medali ya fedha.

 

Video: JPM alivyoiteka Tanga, wananchi walilia kumuona
Eminem kuangusha 'mzigo mzito' mwaka huu, kumfukuzia Jay Z