Mlinda mlango wa klabu ya Liverpool Simon Mignolet, anakaribia kukamilisha mpango wa kuihama klabu hiyo ya Anfield na kujiunga na SSC Napoli ya Italia.

Mlinda mlango huyo kutoka nchini Ubelgiji, ameshindwa kurejea katika kikosi cha kwanza cha majogoo hao wa jiji tangu mwanzoni mwa msimu uliopita na anaamini hatua ya kuihama klabu hiyo itakua suluhisho la kurejea langoni na kucheza mara kwa mara.

Mignolet huenda akakamilisha taratibu za kujiunga na SSC Napoli siku ya Ijumaa, na anapewa nafasi kubwa ya kucheza mchezo wa ufunguzi wa ligi ya Italia siku ya jumamosi dhidi ya SS Lazio.

Kusajiliwa kwa mlinda mlango kutoka nchini Brazil Allison Becker aliyotokea AS Roma kwa ada ya Pauni milioni 67 mwezi uliopita, kumeendelea kuhatarisha nafasi ya Mignolet kurejea langoni mwa Liverpool.

Msimu uliopita Mignolet alipoteza nafasi ya kuwa chaguo la kwanza, kufuatia kiwango kizuri kilichoonyeshwa na Loris Karius, ambaye hata hivyo alishindwa kuendeleza umahiri wake na kusababisha timu ya Liverpool kupoteza mchezo wa fainali ya ligi mabingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid mwezi Mei, kufuatia uzembe aliouonyesha.

Mignolet mwenye umri wa miaka 30, amekua na klabu ya Liverpool tangu mwaka 2013, na tayari ameshacheza michezo 200.

Mwanaume: Usikubali kumwacha mwanamke mwenye tabia hizi
Mfumo wa Maurizio Sarri wamkimbiza Bakayoko