Siku moja baada ya kusimamishwa ili kupisha uchunguzi ufanyike dhidi yake, aliyekua kaimu katibu mkuu wa Young Africans Wakili Simon Patrick, amefunguka mauzauza yaliyopelekea kukumbwa na kadhia hiyo.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa, kamati ya Utendaji ya Young Africans ilifikia maamuzi ya kumsimamisha kazi wakili Simon Patrick, ambaye pia ni  Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama ndani ya klabu hiyo kongwe.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya kikao cha dharula cha Kamati ya Utendaji kilichokaa Novemba 17, 2020 juzi Jumanne ambacho kilifanyika maalum kwa ajili ya kusikiliza shutuma ambazo amehusishwa nazo.

Simon anatumhumiwa kuwa na ukaribu na baadhi ya viongozi wa Simba hali ambayo imewafanya viongozi wa Young Africans kuwa na wasiwasi naye.

Hata hivyo wakili Simon amekiri kukutana na mtendaji mwenye cheo kama chake kutoka Simba SC, lakini hakukua na lolote la hujuma lililozungumzwa baina yao.

“Nakiri kukutana na  Mtendaji mwenye rank kama Yangu kama alivyotaja maeneo ya Yatch Club, lakini sio vikao vya siri kwani kilichonikutanisha nae mtendaji huyo ni suala muhimu ambalo viongozi watatu walinituma na baada ya kikao hicho nilirejesha taarifa na hii naongelea ilikuwa Oktoba 20, 2020”.

Katika hatua nyingine wakili Simon anahisi mpango wa kusimamishwa kwake, huenda ikiwa ni janja janja ya kutaka kumuondoa katika majukumu yake ndani ya Young Africans.

Amesema anahisi mpango huo upo, na huenda nafasi yake akapewa Senzo Mazingiza Mbatha ambaye kwa sasa ni mshauri mkuu wa klabu.

“Mimi nakaiumu nafasi  ya katibu mkuu kwa muda lakini nimeajiriwa kama Mkurugenzi wa Sheria, hivyo basi siwezi kumuhofia Mr Senzo kwani yeye sio mwanasheria bali ni mshauri mkuu wa klabu, kukaimu nafasi maana yake ni unashikiria kwa muda viongozi wanaweza kupiga simu moja tu kwamba kuanzia leo sio kaimu tena na nikatii hofu sijui inatokea wapi.

Suala lingine ambalo wakili Simon anatuhumiwa nalo ni kuhujumu kesi ya Bernard Morrison, kufuta kesi hiyo Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kutopokea simu za Mwenyekiti wake Mshindo Mbete Msolla.

Niyonzima anusurika ajali jijini Kigali
Sirro awaita Lissu, Lema