Kampuni ya simu ya BlackBerry, imesitisha huduma zake ikiwemo kupiga simu, kutuma ujumbe ama kujiunga na intaneti.

Kampuni hiyo ilisitisha huduma zake siku ya Jumanne, Januari 4, na kusema kuwa itaacha kutumia vifaa vyake vinavyotumia BlackBerry 10, 7.1 OS na matoleo yote ya awali.

Hiyo ikiwa na maana kuwa vifaa vyake vya zamani ambavyo havitumiki kwenye programu ya Android havitaweza tena kutumia data, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi, kuunganisha mtandao ama kupiga simu.

Simu hiyo ambayo ilikuwa maarufu wakati simu janja zilipokuwa zinaanza kutumika kwa wingi miaka ya 2000 na kupendelewa na watu maarufu kama vile Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, sasa haitakuwa sokoni.

Toleo la mwisho la mfumo wake wa uendeshaji uliozinduliwa mwaka wa 2013 na uamuzi wa kusitisha simu zake unatoa tafsiri ya mwisho wa teknolojia kongwe.

Mnamo Septemba 2020, kampuni hiyo ilitangaza kusitisha huduma zake kama sehemu ya juhudi zake za kuangazia kutoa programu na huduma za usalama kwa wafanyabiashara, mashirika na serikali kote ulimwenguni chini ya jina BlackBerry Limited.

Young Africans yasaini dili nono Dar es salaam
Super Eagles yafanya mabadiliko AFCON 2022