Msanii Mkongwe wa BongoFleva, Khalid Mohamed maarufu kwa jina la TID au Mzee Kigogo amesema hayupo tayari kuoa kwa sasa kama wasanii wenzake wanavyofanya kwa madai wengi wao wanatumia ndoa kama kutengeneza kiki katika mitandao ya kijamii na sehemu zinginezo.

Ameyasema hayo baada ya kupita takribani siku 24 tokea msanii huyo kutangaza wazi kuwa yupo katika mahusiano na mwanadada mmoja ambae alikuwa nae nchini Ujerumani jambo ambalo wengi walitarajia akitangaza ndoa siku chache zijazo.

“Sijasema kama ninaoa mwezi wa sita (Juni) ila tulikuwa tunajifurahisha mimi na rafiki yangu usingizi katika ‘comment’ instagram ilikuwa utani tu sijafikilia kuwa hivyo. Unajua sasa hivi watu wanataka kutengenezea kama kiki kitendo cha kuoa, kwa hiyo mimi sio mtu kutafuta kiki kwa kutumia ndoa,”amesema TID

Hata hivyo, Mbali na hilo, TID hakusita kutoa siri za swahiba wake wa miaka mingi Q-Chief kwamba alishawahi kutangaza kutaka kuoa lakini mpaka sasa hakuna chochote alichokifanya.

Video: Mbarawa apangua hoja za wabunge, Sakata jipya la trilioni 1.8/-
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 26, 2018

Comments

comments