Uongozi wa Singida Big Stars, umeweka wazi kuwa, unahitaji kufanya vizuri kwenye mashindano inayoshiriki ikiwa ni pamoja na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Afisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza, amesema kuwa kila mashindano kwao ni muhimu na wanafanya maandalizi mazuri kupata matokeo bora.

“Tuna kazi kubwa kwenye mashindano ambayo tunashiriki na kila mchezaji anatambua kuwa ushindani ni mkubwa, tutapambana kufanya vizuri kila mashindano tunayoshiriki.”

“Ambacho tunahitaji kwenye mashindano tunayoshiriki ikiwa ni ligi pamoja na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ mipango yetu ni kupata matokeo mazuri,” amesema Masanza.

Singida Big Stars mchezo wa Robo Fainali ya ‘ASFC’ inatarajiwa kucheza dhidi ya Mbeya City, Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Liti, mjini Singida. Mshindi wa mchezo huo anatarajiwa kukutana na mshindi kati ya Young Africans na Geita Gold kwenye Hatua ya Nusu Fainali.

Robertinho: Tutaiheshimu Raja Casablanca
Matariji wapishana kuinunua Man Utd