Klabu ya Singida Big Stars imetangaza kukamilisha Dili la Usajili wa Kiungo Aziz Andabwile Mwambalaswa, akitokea Mbeya City FC ya jijini Mbeya.

Singida Big Stars imetoa taarifa ya usajili wa Kiungo huyo, na kuanika picha katika Mitandao ya Kijamii akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Muhibu Kanu.

Singida Big Stars imetangaza usajili huo katika kurasa zake za Mitandao ya kijamii huku ikimwagia sifa Kedekede kiungo huyo ambaye aliwahi kucheza soka nje ya nchi.

Ujumbe wa Klabu hiyo itakayocheza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2022/23 umeandikwa: RASMI: Aziz Andabwile ni BIG STAR ✅️

Ni kiungo mwenye uwezo wa kucheza nafasi tofauti tofauti uwanjani. Mchezaji kijana, mzawa, msomi, mpambanaji wa kweli akiwa na timu yake mpaka timu ya Taifa.

Pia ni mtaalamu wa pasi na mashuti ya mbali. Ameshacheza Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na timu ya Big Bullet ya Malawi.

Kwa sasa ni Kiungo Mkabaji anayetegemewa na Timu ya Taifa

Habari kuu kwenye magazeti ya leo July 2, 2022    
Tuzo 2021/22 kutolewa Julai 07 Dar es salaam