Afisa Habari wa Singida Big Stars Hussein Massanza Jr, amewashukua baadhi ya Mashabiki wa Soka La Bongo wanaoendelea kuhoji Klabu hiyo kumtoa kwa mkopo Mlinda Lango Metacha Mnata, aliyesajiliwa Young Africans.

Mlinda Lango huyo alikamilisha taratibu za kujiunga na Young Africans kwa Mkataba wa Mkopo dakika chache kabla ya kufungwa kwa Dirisha Dogo la Usajili, Jumapili (Januari 15).

Massanza Jr amesema, anashangazwa kuona mijadala ikiendelea katika Mitandao ya Kijamii kuhusu Biashara ya usajili wa Mlinda Lango huyo kwenda Young Africans, wakati Uongozi wa Klabu ya Singida Big Stars imefanya hivyo kwa wachezaji wengine kujiunga na Klabu za Ligi Kuu.

Amesema huenda baadhi ya Mashabiki wa Soka La Bongo wana kasumba ya kuichukia Young Africans hasa inapofanya Biashara ya Usajili na Singida Big Stars.

“Tumewatoa wachezaji wengi tu kwa mkopo, na kwenda timu mbalimbali, Shida mchezaji akienda Yanga inakuwa kelele, timu nyingine kimyaaaa”

“Kyombo karudisha hela kaenda Simba.. Kimyaaa, Sabato Polisi Tz.. Kimyaaa, Kotei Mtibwa… Kimyaaa, Msuva Mbeya City Kimyaaa”

“Tumemsajili Kagere, Wawa, Ndemla.. Wote walipita Simba.. Kimyaaaa”

“Mna shida gani kwani ni vibaya kufanya biashara na Yanga?” amesema Hussein Massanza Jr

Tayari Metacha Mnata ameshajiunga na Kikosi cha Young Africans na kuanza mazoezi ya wachezaji wenzake kambini Avic Town, Kigamboni jijini Dar es salaam.

Usajili wa Mlinda Lango huyo ambaye aliwahi kupita Young Africans, ulilazimika kufanyika kutokana na Mlinda Lango namba mbili Abutwalib Hamad Mshery kuendelea kuwa majeruhi.

Waziri Mkuu atangaza kung'atuka mwezi Februari
Mawaziri watatu wafariki kwa ajali ya Chopa