Uongozi wa Klabu ya Singida United umesema kuwa utapambana kadri ya uwezo wao katika michuano ya ligi kuu ili historia yao iweze kubaki salama huku wakiwatishia wapinzani wao Mbeya City kwamba wao sio ngazi ya kuwapandisha wengine daraja.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga ikiwa zimebaki saa kadhaa kuelekea katika mtanange wao dhidi ya Mbeya City leo Aprili 27, 2018 katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania Bara.

“Tunaenda kucheza na Mbeya City tukiwa tunawaheshimu kwani wametoka sare na timu kubwa kama Yanga hivyo naamini hata sisi wametupania na pia wanahitaji kujiondoa katika nafasi waliyopo, lakini sisi sio ngazi ya wengine kung’ang’ania kutokushuka daraja. Sisi tunacheza mpira na hatuingii uwanjani kumpa mpinzani wetu pointi tatu bali tunapambana,”amesema Sanga

Hata hivyo, Singida United inashuka dimbani ikiwa nafasi ya tano huku ikiwa na alama 37 kwa michezo 25 katika msimamo wa ligi kuu, Mbeya City iko nafasi ya 10 kwa alama 26 yenyewe ikiwa na michezo 24 mpaka sasa waliyofanikiwa kuicheza.

Zidane asema haikuwa rahisi kuifunga Bayern Munich
Rais Kim Jong Un afanya ziara Korea Kusini