Klabu ya singida united imefanya usajili wa wachezaji watatu akiwemo mshambuliaji chipukizi Tibar John kutoka Ndanda FC ya Mtwara kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kinda huyo aliyefanya vizuri kwenye ligi kuu ya Tanzania bara ametambulishwa mapema leo na uongozi wa timu hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika  kwenye Hoteli ya Naura-Spring  jijini  Arusha.

Aidha, Klabu hiyo imewatambulisha wachezaji wengine wawili wapya ilio wasajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi akiwamo Diaby Amara kutoka Ghana na Felipe Oliveira kutoka Brazil.

Mkurugenzi mtendaji wa timu hiyo Festo Sanga akimzungumzia mchezaji  Felipe kutoka Brazil,  amesema ni mchezaji ambaye wamejiridhisha anaubora wa kuitumikia timu hiyo na ametoka moja kwa moja nchini brazil katika jiji la Sao Paulo na kuja nchini.

‘’ni mchezaji ambaye ametokea Brazil,  ameingia nchini ana wiki mbili kwa maana anafanya mazoezi na wenzake, kikubwa  ni sisi tunatamani kumuona anafanya nini kwenye mashindano ya sportpesa ili tusaini makubaliano naye’’ amesema  Festo Sanga.

Singida United inatarajia kushiriki mashindano  ya Sportpesa yanayotarajia kuanza kutimua vumbi nchini Kenya hivi karibuni na kushirikisha timu nane, zikiwemo nne kutoka Kenya ambazo ni Gor Mahia Fc,  AFC Leopards, Kariobangi Sharks, Kakamega Homeboyz  na tatu kutoka Tanzania bara ambazo ni Simba SC, Yanga FC,Singida United pamoja na  JKU kutoka visiwani Zanzibar.

Wazazi St. Florence waanza kuhamisha watoto wao
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Nigeria