Kocha Mkuu wa Singida United, Ramadhani Nswanzurwimo, amesema kikosi chake kitaendelea kupambana kusaka ushindi katika mihezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo kutroka nchini Burundi amesema bado hajakata tama ya kupambana katika ligi hiyo, licha ya timu yake kushuka daraja ikiwa ina michezo kadhaa mkononi.

Amesema wachezaji wake ambao ni vijana waliobakia kwenye kikosi hicho, wanaendelea kuimarika na michezo inayofuata watahakikisha wanapambana bila kuchoka.

“Wachezaji wangu bado hawana muunganiko mzuri, ni vijana na hawana pia uzoefu mkubwa wa kupambana kwenye ligi, ninaamini wanaendelea kujifunza na kuimarika,” alisema kocha huyo.

Mwishoni mwa juma lililopita Singida United walikubali kufungwa mabao saba kwa sifuri mbele ya Azam FC waliokua nyumbani Azam Complex, Chamazi – Dar es Salaam.

Singida United inaburuza mkia ikiwa na pointi 15 baada ya kushuka dimbani mara 33 wakati tayari bingwa wa msimu huu, Simba anakabidhiwa kombe kesho mkoani Lindi. Leo Jumatano Singida United itashuka dimbani kwenye Uwanja wa Azam Complex kuwakabili KMC.

Kocha Sven, Bocco wawaahidi jambo wana Simba SC
Kenya kufungua shule 2021