Klabu ya Singida United FC Usiku wa kuamkia leo ilifunga dirisha la usajili kwa kukamilisha mpango wa kumnasa mshambuliaji waKaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Mzimbabwe Michelle Katsavairo.
Katsavairo mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Singida United kwa mkopo wa msimu mmoja, hii ni baada ya kushindwa kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Kaizer Chiefs.
Kabla ya kutua Kaizer Chiefs, Katsavairo aliwahi kutamba na vilabu vya nyumbani kwao Zimbabwe vya Platinum FC pamoja na Chicken Inn F.C.
Mbali ya Katsavairo mwingine aliyenaswa na Singida United siku ya mwisho ya usajili ni  mlinda mlango Peter Manyika Jr aliyekuwa akiichezea Simba.
Manyika amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba wake na Simba kufikia kikomo.
Wakati huohuo Singida United imemtoa kwa mkopo wa msimu mmoja kwenda Stand United nyota wake Mzimbabwe, Wisdom Mutasa.

Lukuvi awaonya matapeli na madalali jijini Dar
Serikali yangu haitawavumilia wavivu-JPM