Beki wa kushoto kutoka Uganda na klabu ya Tusker FC ya Kenya, Shafik Batambuze amesaini kandarasi ya awali ya miaka miwili ya kuitumikia klabu ya Singida United ya mkoani Singida, ambayo itashiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2017/18.

Batambuze mwenye umri wa miaka 22 ameingia kandarasi hiyo jijini Nairobi, Kenya baada ya kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga.

Batambuze alitua ligi kuu ya soka ya Kenya mwaka 2012 na kujiunga na klabu ya Muthoroni Youth akitokea Simba ya nyumbani kwao Uganda. Pia alizichezea klabu vya Western Stima na Sofapaka kabla ya kujiunga na Tusker FC.

Mwaka jana Batambuze aliisaidia Tusker FC iliyokuwa ikinolewa na Mganda, Paul Nkata kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Kenya na kumaliza ufalme wa miaka mitatu wa Gor Mahia.

Mafaniko hayo yalimpa Batambuze nafasi ya kuiwakilisha Uganda kwenye michuano ya AFCON iliyofanyika Januari mwaka huu nchini Gabon.

Batambuze anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Singida United baada ya Wazimbabwe, Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Twafaza Kutinyu.

@

Video: Jumia mobile week kuanza mei 22
Infantino afanya mabadiliko makubwa ndani ya FIFA