Uongozi wa klabu ya Singida Utd umeendelea kukamilisha ndoto za klabu hiyo itakayocheza ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2017/18, baada ya kupanda daraja ikitokea ligi la kwanza msimu uliopita.

Uongozi wa klabu hiyo ya mkoani SIngada hii leo umekamilisha mpango wa kununua basi la usafiri kwa ajili ya kikosi chao pindi kitakapokua kwenye heka heka za kushiriki ligi kuu pamoja na kombe la shirikisho.

Mkurugenzi wa Singida Utd Festo Richard Sanga, amesema ununuzi wa basi hilo ulikua ni moja ya mikakati yao waliyojiwekea baada ya kupanda daraja, na wanaamini bado kuna mahitaji mengine wataendelea kuyakamilisha kutokana na mipango waliyojiwekea.

Utambulisho wa basi hilo lenye thamani ya Shilingi Milioni 330 umefanyika kwenye hoteli ya Lamada iliyopo Ilala jijini Dar Es Salaam na kushuhudiwa na waandishi wa habari.

Sandro Ramirez Atua Goodison Park
Jeff Horn awapa neno wanaodai hakumpiga Manny Pacquiao