Kiungo wa klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,  Siphiwe Tshabalala amejiunga na timu iliyopanda daraja kucheza ligi kuu nchini Uturuki, BB Erzurumspor.

Kaizer Chiefs imeweka wazi kuwa wamefikia makubaliano ya kumuachia mchezaji huyo aliyeitumikia  chiefs tangu mwaka  2007 na kufanikiwa kucheza michezo 372 na kufunga mabao 58.

Tshabalala amesema anayofuraha kujiunga na timu hiyo kwa kuwa tangu zamani ndoto yake ni kucheza soka barani ulaya.

“Nataka niwashukuru mashabiki kwa upendo na amani ilikuwa ni safari nzuri kwa takribani miaka 12 nimefurahia kila dakika kucheza Kaizer Chiefs ’’ amesema Tshabalala

“Mara zote nilitaka kucheza ulaya, na sikuwahi kuona aibu kusema kuhusu hilo, ilikuwa itokee tangu zamani Iakini hiyo nimipango ya mungu,’’ ameongeza Tshabalala.

Aidha, kiungo huyo wa timu ya taifa ya Afrika kusini ‘Bafana Bafana’ anakumbukwa kwa kuweka historia ya kufunga bao la kwanza kwenye Michuano ya kombe la dunia 2010 kwenye ardhi ya nyumbani dhidi ya Mexico, mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Liverpool kuangukia kundi la kifo?
Yametimia: Mariano Díaz Mejía arejea Santiago Bernabeu