Fununu zinadokeza kuwa, kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ametakiwa kumpiga tafu Louis Van Gaal.

Imeelezwa kuwa, mabosi wa klabu hiyo ya Old Trafford wametishwa na mwenendo wa timu hiyo na wanahofia kumfukuza kazi kocha wao ili kutotibua zaidi mambo.

Imedaiwa kuwa Ferguson aliketi na Makamu Mwenyekiti wa United, Ed Woodward na Mtendaji Mkuu wa zamani wa klabu iyo, David Gill hapo Old Trafford mwishoni mwa wiki.

Ferguson kocha aliyeipa timu hiyo mafanikio yasiyo kifani katika miaka 27 aliyoiongoza, hajasema lolote kuhusu tetesi hizo za kutakiwa umsaidia Van Gaal.

ZFA Wilaya Ya Mjini Walia Na Kombe La Mapinduzi
Ronaldo Achoshwa Na Matusi Ya Mashabiki