Imeelezwa kuwa unywaji wa maziwa kwa watu wenye umri mkubwa huzuia maumivu ya misuli na kurudisha ute uliopotea kwenye misuli.

Meneja vyanzo vya maziwa wa kiwanda cha kuzalisha maziwa cha Tanga Fresh, Annadomana Nyanga, amebainisha hay o alipozungumza na waandishi wa habari na watafiti waliokuwa katika mafunzo ya habari za kisayansi yaliyoendeshwa na Tume ya sayansi na Teknolijia mkoani Tanga.

Nyanga amesema kuwa tafiti zinaonesha maziwa yana wingi wa madini ya Protini ambayo yanasaidia kuimarisha mifupa hasa kwa wazee na watoto.

Amesema iwapo wazee watakunywa maziwa katika kiwango stahiki, wataepukana na uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya mifupa ambao umekuwa changamoto kuwa kwao.

Kifungo miaka 60 kwa kuvutisha bangi watoto

“Tatizo kubwa lililopo, watanzania hatuna utamaduni wa kunywa maziwa, takwimu zinaonesha mtu mmoja anastahili kunywa lita 100 kwa mwaka, mpaka sasa watanzania wanakunywa lita 47 pekee kwa mwaka ” alisema Nyanga

Aidha amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye mpango wa kuwaelimisha wafugaji namna bora ya ufugaji ambao utaongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Kipa bora azawadiwa bunduki aina ya AK-47
Washtakiwa wa kigeni wakwamisha kesi ya “MO”