Rais wa zamani wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf ameshinda tuzo ya mwaka ya ‘Mo Ibrahim’ kwa Uongozi wa Afrika ambayo hupewa viongozi walioonekana kuwa na utawala bora unaofuata misingi ya katiba na kuheshimu haki za binadamu.

Ellen Johnson Sirleaf amekuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya Urais mwaka 2006 na kumaliza muda wake mwezi uliopita baada ya kuitumikia nchi yake kwa mihula miwili.

Aidha, Kamati tendaji ya tuzo ya ‘Mo Ibrahim’ imesema kuwa, Ellen Johnson Sirleaf ameonyesha uongozi wa kipekee katika kukabiliana na changamoto zilizowahi kutokea katika awamu zake mbili za uongozi alipokuwa Rais wa Liberia.

Wakati anaingia madarakani mwaka 2005, nchi hiyo ilikuwa imegawanyika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka kadhaa na tuzo hiyo ya amani ilikuwa ni kwa ajili ya kumpongeza kusaidia kuiimarisha demokrasia na kuwaunganisha wananchi wa nchi hiyo.

Hata hivyo, wakosoaji wake wamekuwa wakimkosoa kwa kuwa na upendeleo, kutokana na kuwachagua watoto wake katika nafasi za ngazi za juu na pia wanadai kuwa hakuchukua hatua za kutosha kupambana na rushwa.

Video: Lowassa akoleza moto waraka wa Maaskofu, Mkuu usalama CDM aanika mbinu sita
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 12, 2018

Comments

comments