Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro, amewaomba viongozi wa dini pamoja na wale wa siasa kulisaidia jeshi la polisi kupaza sauti na kutoa elimu juu ya mambo ya ubakaji jambo ambalo linaonekana kuenea kwa kasi.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa matukio ya kubaka yamekuwa changamoto kubwa kuliko uhalifu wa uporaji na matukio mengine.

Amesema kuwa matukio ya ubakaji yameenea kwa kasi kutokana na mmomonyoko wa maadili, ambapo amewaomba viongozi mbalimbali wa dini na jamii kwa ujumla kuingilia kati suala hilo ambalo linaonekana kuwa sugu kwasasa.

Aidha, amesema kuwa wapo wanaume wenye umri mkubwa lakini bado wanatoka kimapenzi na watoto wenye umri chini ya miaka 18 pasipo kujua kwamba hata kama ameridhia bado hilo ni kosa kisheria,

Hata hivyo, ameongeza kuwa jeshi la polisi kwasasa linajipanga kuhakikisha kwamba wanatoa elimu mashuleni ili kuweza kuwajengea uelewa wanafunzi waweze kuepuka ulaghai wanaokumbana nao.

 

Nimerudi nyumbani, sijutii kurudi CCM- Lowassa
Mwili wa marehemu Ruge Mutahaba wapokelewa jijini Dar