Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema takribani Askari Polisi wanafunzi 156 wamefukuzwa mafunzo ya kijeshi kutokana na sababu ikiwemo utovu wa nidhamu.

IGP Sirro, amesema hayo katika ziara yake ya kutembelea uwanja wa medani za kivita wilaya ya Siha, West Kilimanjaro katika Shule ya Polisi na kusema baadhi ya makosa yaliyosababishwa kufukuzwa ni pamoja na utovu wa nidhamu na kufanya mambo yasiyokubalika ndani ya shule ya Polisi.

Hata hivyo, IGP Sirro amewataka Wanafunzi hao wa kozi ya awali ya Askari Polisi kufuata sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ikiwa pamoja na kudumisha nidhamu ndani ya Jeshi la Polisi.

Vigogo CWT kurejesha pesa, jela yawahusu
Try Again amaliza mikwaruzano Simba SC