Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam wanatarajia  kufanya operesheni kubwa ya kukamata wahalifu katika maeneo korofi ya jijini humo.

Hayo yamesemwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro, aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa ziara ya siku kumi ya Mkuu wa mkoa  huo Paul Makonda,

“Nawaomba wazazi wa Dar es salaam, wachungeni watoto wenu na kuwalea katika maadili, kama ni wahalifu, wakorofi lazima tuwakamate, tunataka kujenga Dar  es salaam mpya ambayo itakuwa salama”alisema Sirro.

Aidha, Sirro aliongeza kuwa Jeshi la Polisi  haliko tayari kuona watu wakiishi kwa hofu katika jiji la Dar es salaam na watahakikisha usalama kwa wakazi wote na mali zao uanpatikana muda wote na kuongeza kuwa wamejipanga vya kutosha kuweza kukabiliana na magenge hayo ya uhalifu.

Hata hivyo Sirro aliyataja maeneo atakayoanza nayo ni pamoja na kata ya kigogo, Manispaa ya Kinondoni, na kuongeza kuwa operesheni hiyo itakuwa kama kimbunga.

Mkaa wageuka dhahabu,Serikali kupandisha kodi
Makinda: Mabadiliko sheria ya ndoa ni muhimu