Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limetangaza orodha ya waamuzi watakaochezesha mchezo wapili wa Nusu Fainali Kombe La Shirikisho Tanzania Bara (ASFC), kati ya Simba SC dhidi ya Young Africans Jumapili, Julai 12.

TFF imetangaza orodha ya waamuzi sita watakaochezesha mpambno huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini na pengine ukanda wote wa Afrika mashariki na kati.

Mara ya mwishoni TFF walitangaza orodha ya waamuzi kama hiyo kwenye mchezo wa Robo Fainali kati ya Simba na Azam FC uliochezwa juma lililopita, ambapo mwamuzi Ramadhan Kayoko wa Dar es salaam aliwaongoza Arnold bugado kutoka Tanga na Frank Komba wa Dar es salaam.

Mashabiki 30,000 kushuhudia Simba SC Vs Young Africans

Katika mchezo wa Jumapili TFF imemtangaza Abubakar Mturo kutoka Mtwara kuwa mwamuzi wa kati, akisaididwa na washika vibendera Abdalah Mwinyimkuu (Singida) na Nadeem Aloyce (Dar es salaam).

Waamuzi wengine ni Frank Komba na Kassim Mpanga wote kutoka Dar es salaam, ambao watakua pembezoni mwa milango ya timu zote mbili.

Miamba hiyo ya soka nchini Tanzania inakwenda kukutana mwishoni mwa juma hili, baada ya kushinda michezo ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho juma lililopita, ambapo kwa upande wa Simba SC waliibamiza Azam FC mabao mawili kwa sifuri, huku Young Africans wakiifunga Kagera Sugar mabao mawili kwa moja.

Wasira: Hata Malaika angegombea na Bulaya 2015 angeshindwa, nagombea tena
Eng Hersi: Ni aibu kwa Young Africans kushindwa kutwaa taji