Watu sita wamefariki katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa Septemba 17,  katika Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma, Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na vifo vya watu sita.

Basi hilo aina ya Coaster lilikua likisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Nyasa,  limepinduka katika mlima Kipololo uliopo Wilayani Mbinga wakati likiwa njiani kuelekea Lundo, Nyasa.

Aidha mganga wa hospitali ya wilaya ya Mbinga, Dk Shila Mishiuya amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kwamba wanasubiri miili  pamoja na majeruhi wa ajali hiyo.

Amesema idadi kamili ya majeruhi bado haijajulikana na kwamba  atatoa taarifa  baada ya kupokea miili na majeruhi wa ajali hiyo.

Wahusika vyeti vya vifo zaidi ya Ng'ombe 270 wasakwa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 17, 2021