Wagonga nyundo wa jijini London, West Ham United wapo tayari kutoa kiasi cha Pauni milioni 30, kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Olympic Lyon, Alexandre Lacazette.

Meneja wa West Ham Utd, Slaven Bilic, amekua mstari wa mbele kushawishi usajili wa mshambuliaji huyo, kutokana na hitaji la kutaka kuona ushindani unaongezeka kikosini mwake, msimu ujao wa ligi.

Awali meneja huyo kutoka nchini Croatia, alionyesha kukata tamaa katika hatua ya usajili wa Lacazette, baada ya kutakiwa kitoa kiasi cha Pauni million 31, lakini amekuja na njia mbadala za kutaka kutoa kiasi cha Pauni milioni 30.

Msimu uliopita wa ligi ya nchini Ufaransa, ilishuhudia Lacazette, akifanikiwa kufunga mabao 23.

Mbunge Wa CCM Amvaa Wa Chadema, Adai 'Ametamani Mwanaume Wa Mtu Mwingine’
Jurgen Klopp Adhamiria Kumsajili Sadio Mane